Sitta Gabu: Aliyesifika kwa Utabiri, Uganga!
Na Charles Kayoka
Nikiwa Bariadi hivi karibuni nikifuatilia nyayo na vituko vya Ng’wanamalundi,( nawashukuru wasomaji walionichagiza kufanya utafiti zaidi na kunieleza wapi pa kwenda,) nikakutana na babu mmoja aliyeniambia kuwa eneo moja linaloitwa Kilulu, kilomita kama tano kutoka Bariadi mjini, kuna eneo la mawe ambako aliwahi kusihi mti anayeitwa Sitta, asili ya kabila la Taturu, ambaye alikuwa bingwa wa kutabiri na uganga pia.
Huyu bwana alikuwa na vituko. Kwa maelezo ya wenyeji taarifa zake ni kuwa alikuwa ana uwezo wa kujua nini kitatokea pale kijijini, au kwa mtu binafsi ambaye atafika kuomba msaada wake. Nilipomuuliza mzee huyu kama huo sio ushirikina alikana kwa nguvu na kusema mtu anakuwa mshirikina kama anaroga watu, sasa kama huyu anatusaidia kujua ya mbeleni na kututibu maradhi ushirikina unatoka wapi. Aidha alisema kuwa kosa kubwa lililofanyika ni kuwa Waafrika hatuwa na elimu na ufahamu wa kuweka kumbukumbu mambo muhimu ya utamaduni wetu.
Wengi wa wenyeji wenye umri zaidi ya miaka hamsini au hata baba zao, hawajawahi kumuona, ila wanajua kuwa aliishi na alama ya kuishi kwake eneo hilo zipo. Tulipofika eneo husika Bibi mmoja wa miaka 60 alikubali kutuongoza katika ziara ile. Alisema kwanza kuwa huyu bwana Sitta alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya maajabu.
Kwanza alikuwa kiboko ya Wamaasai waiba ng’ombe. Alipojiwa na taarifa (ndoto) kuwa kutatokea uvamivi wa waiba ng’ombe aliwabadilisha wanyama wake kuwa mawe. Tulipofika eneo hilo tukafikishwa kwenye nyumba ya mmoja wa waganga anaye endelea kuishi hapo (ni kaya pekee iliyopo neo hilo). Mtoto wake akatupeleka eneo ambalo kuna jiwe lenye mfano wa ng’ombe. Alisema taarifa za Sita zimesafiri katika vichwa vya watu kwa muda mrefu hata ukweli kamili sasa si rahisi kuupata. Alisema ni kweli alikuwa anabadilisha ng’ombe na mbuzi kuwa mawe lakini ushahidi pekee ni hilo jiwe, inawezekana kuwa mawe mengi ya pale ni sehemu ya wanyama aliwabadilisha kabla ya kufa kwake.
Bibi aliyetusindikiza alisema nay eye aliliona jiwe lile kwa mara ya kwanza siku ile ingawa habari zake alikuwa akizisikia tangu alipokuwa mdogo, na visa vya Sita Gabu anavijua. Tukapelekwa eneo la kaburi lake, limefukiwa kwa alama yam awe mengi na pembeni kulikuwa na jiwe lililoandikwa karibu kwa Sitta Gabu. Eneo hilopalikuwa na nyumba yake lakini sasa hakuna hata dalili. (inasemekana aliishi karne ya kumi na tisa mwishoni kuelekea mwanzo wa karne ya ishirini). Eneo hilo tukakuta vibuyu na majivu, ishara ya kuwa matambiko yanaendelea kufanyika kwa kufuata imani juu ya huyu bwana.
Baadaye tukaonyeshwa eneo ki mlima cha mawe kilicho na wastani wa urefu wa mita hamsini hivi. Tukaambiwa kuwa siku zingine Sita alikuwa akipanda kule kwenye kilele cha kilima na kigoda chake na kukaa huko yeye na mkewe wakichunga ng’ombe zake. Namna gani alipanda hakuna anayeweza kujua lakini tulionyeshwa alama ya ngazi ambayo kwa kweli huwezi kupanda. Na kule kwenye kile alitoboa matundu mawili ya kuwekea miguu yake ili isining’inie wakati anapumzika. Na chini yam lima huo kulikuwa na jiwe ambalo lina ishara ya simba. Lakini kutokana na wingi wa umri na kuharibiwa na mvua na upepo, huwezi tena kuitambua kwa urahisi. Chini pembeni yam lima huo kuna bao la jiwe kubwa kwa ajili ya mchezo wa solo. Kuwa alikuwa akija na marafiki zake kucheza solo kwenye jiwe lile. Na mbali na hapo kuna kisima ambacho maji yake hutoweka na kisima kukauka kama wewe ni mtu mwenye nia mbaya. Hatukufika kwa sababu usiku ulishafika tulipaswa kuondoka. Linguine ni kuwa kabla yay eye na mkewe kufa alitengeneza sanamu yake na mkewe kwenye jiwe kubwa. Nayo inapotea kutokana na uchakavu wa jiwe lile ambalo sio gumu sana. Mama mmoja anasema alipokuwa mdogo yeye na wanafunzi wenzake walikuwa wanakuja eneo hilo kushuhudia maajabu ya Sitta Gabu. Lakini kutokana na kutotunzwa mvua, upepo, mchanga na mifumo mingine ya hali ya hewa inapachakaza mahali hapa. Kwani hata hilo bao limebaki vialama tu. Lakini ni ushahidi kuwa karne za huko nyuma watu walikuwa wakishindana kwa uwezo wa uganga na ulozi.
pix. i. The rock on which the great witch, Gabu Sitta was Sitting overlooking his flock of animals.
The burial place of Gabu Sita. Now a witcraft shrine. Burried 100 years ago
No comments:
Post a Comment